Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Kim Simplis Barrow, Mke
wa Waziri Mkuu wa Belize na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia masuala ya Wanawake na Watoto. Mama Barrow kwa
kushirikiana na Umoja wa Mataifa ndio walioandaa mkutano wa Wake wa
Marais na Wakuu wa Nchi kuzungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na
wasichana kifedha.na “First Ladies Global Call to Action Conference on Women and Girls’ Financial Health.” Tarehe 25 Septemba,2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye mkutano wa Wake wa
Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa uliozungumzia masuala ya
kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York Marekani tarehe
25.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mama Joyce Banda
(kushoto) na wa kwanza kulia ni Mama Dianne Stewart, Mkurugenzi wa Idara
ya Habari na Uhusiano wa Shirika la United Nations Populations Fund
akifuatiwa na Bi Mpule Kwelagobe, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa
MPULE Institute for Indogenous Development. 
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa
Nchi za Umoja wa Mataifa. Kutoka kushoto ni Mama Kim Barrow, Mke wa
Waziri Mkuu wa Belize, Mama Joyce Banda na wa kwanza kushoto ni Mama
Dianne Stewart. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI