Sina shaka umewahi kusikia watu wengi wakilalamika kuwa akaunti zao za barua pepe zimekuwa ‘hacked’ na matapeli wa mtandaoni, ambao husambaza e-mail ya kuomba msaada wa pesa kwa watu wote ambao wako kwenye contacts za mwenye email husika. Director wa video, Adam Juma leo
amekuwa muhanga wa tukio kama hilo baada ya mtu asiyefahamika kufanikiwa kuingia kwenye akaunti yake na kusambaza ujumbe wa kuomba msaada wa fedha kwa watu ambao Adam huwasiliana nao.
Kupitia Instagram Adam ametoa tahadhari:
“Dahhhh! Kuna mtu kahack account ya email, ukiona ujumbe unaomba hela ujue sio mimi! Very sad aisee”.
HABARI PICHA NA BONGO 5/wamburababu blog