RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA MJINI DUBAI WAKIWA NJIANI KUREJEA NYUMBANI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai waliposimama kwa
muda wakiwa
njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani,
walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika
ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
Mama
Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa
njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani,
walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika
ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia ni Balozi Mdogo wa Tanzania,
Dubai, Mhe Omari Mjenga.
Balozi
wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Mbarouk Nassor
Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe. Mohamed Gello katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika
kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama
kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria
mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais
BArack Obama wa Marekani.
(Picha na IKULU)