Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada wa
chakula kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma
chenye thamani ya Dola ya Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3
Bilioni, ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan. Kushoto ni Balozi wa
Japan nchini, Masaki Okada na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Chakula Duniani (WFP), Richard Regan. Waziri Chikawe alipokea msaada huo
na kumkabidhi Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa WFP, Regan, Bandari ya Dar
es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akipokea galoni
ya mafuta ya kula kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada
(kushoto) ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya chakula cha msaada kwa
ajili ya Wakimbizi kilichotolewa na Serikali ya Japan. Kulia ni
Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard
Regan akipokea msaada huo kutoka kwa Waziri Chikawe ambao una thamani
ya Dola za Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 bilioni katika
tukio la makabidhiano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimshukuru
Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) kwa msaada wa chakula
wenye thamani ya Dola za Marekani 1.4 milioni ambao ni sawa na Shilingi
2.3 Bilioni ambao Serikali yake imetoa kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi
ya Nyarugusu, mkoani Kigoma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Chakula Duniani (WFP), Richard Regan ambaye alikabidhiwa msaada huo
baada ya Waziri Chikawe kuupokea katika sherehe fupi ya makabidhiano
iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI