Rais wa Marekani Barak Obama amesema nchi yake inajiandaa kusaidia kumaliza mgogoro katika Gaza kati ya Israel na Hamas.
Katika
mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu Benjamini Netanyahu, Rais Obama
amesisitiza umuhimu wa pande zote mbili kuepuka mashambulizi zaidi ili
kurudisha utulivu. Hapo awali, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki
Moon, ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa lililoitishwa kwa
dharura kuwa matumizi makubwa ya nguvu hayavumiliki na wanaoumia ni
wananchi.(P.T)
Naye
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema mashambulizi katika
Gaza yataongezeka. Maafisa wa afya wanasema zaidi ya watu 80
wameshapoteza maisha tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israeli katika
eneo hilo la gaza.
" Mpaka
sasa mapambano yanaendelea kama yalivyopangwa lakini tunaweza kutegemea
mengine siku za usoni. Mpaka sasa tumeshaipiga Hamas na mashirika ya
kigaidi na tutaendelea kuongeza nguvu dhidi yao kadri mapambano
yanavyoendelea" Alisema Netanyau
Kwa
upande wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas anasema anayo taarifa kuwa
Israel wanampango wa kuendesha oparesheni ya ardhini katika eneo la Gaza
saa chache zijazo.
"serikali
ya Israel imesema itafanya oparesheni ya ardhini katika ukanda wa Gaza,
ambayo itaanza muda mchache ujao. Asubuhi hii tumetaarifiwa kuwa wakazi
wa mpakani katika eneo la Gaza, Beit Hanoun na Beit Lahiya pamoja na
vijiji na miji mikubwa walitakiwa kuondoka kuelekea katika maeneo ya
katikati" Alisema Rais Mahamamod Abas
Chanzo:BBC