
Kati
ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa
maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali.
Mwaka
huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na
changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
Kwanza
Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na
baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya
kufurahisha.
Zaidi
ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha
mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji
vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa
majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo
![]() |
Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya
|
![]() |
Na
mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye
makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya
|
![]() |
Mtaalamu wa mapambo yatokanayo na shanga na usimamizi wa filamu nchini Kenya Emmah Irungu.
|
![]() |
Mwandishi wa habari kutoka Kenya BMJ Mureithi
|



