Hakuna biashara kila mtaa uligeuka kuwa mchungu.
hapakaliki hapa
Oparesheni ofisa wa zima moto, Sajenti meja Gadafi Masoud amesema msikiti wa Hindu wanaosali masinga singa umenusurika kuchomwa moto na machinga hao baada ya magari makubwa mawili kikosi chake kuuzima moto uliowashwa na wamachinga kwa lengo la kuuteketeza msikiti huo ulio katika eneo waliloondolewa
mtaa kwa mtaa hapatoshi
hakuna cha gari wala mtu hata ndege wa anagani walitoweka kabisa
tunawafata huko huko
Vijana waandamanaji wakifunga barabara, ingawa kuna walakini je hawa nao ni machinga? Abdukadri Salim anasema kuwa vijana wanatumiwa kufanya vurugu na siyowamachinga
Jeshi la polisi katika doria mtaa kwa mtaa.
Jeshi la wananchi lilitoa askari wake wa kijeshi “MP” kuimarisha ulinzi kwenye vitengo vya mabenki, ofisi za serikali na maeneo nyeti ili kutokwaza shughuli za kila siku kuendelea.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola hakuweza kupatikana kwa kuwa yuko safari kikazi na msaidizi wake Christopher Fuime alidaiwa kuwa katika oparesheni hiyo huku baadhi ya askari ambao hawakutaka kutajwa majina yao wakisema zaidi ya wamachinga 40 wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.
KATIKATI ya jiji la Mwanza leo paligeuka kuwa pachungu baada ya mabomu zaidi ya 120 kulindima toka saa 3:58 asubuhi hadi 8:45 na kulifanya eneo hilo lisikalike.
Mabomu hayo yalilindima maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo eneo maarufu la Makoroboi kufuatia kuvunjwa kwa vibanda vya machinga jana asubuhi hali iliyowafanya wacharuke na kuanza mapambano na askari polisi na mgambo wa Jiji huku wakishinikiza wenzao walio kwenye maeneo halali nao waondolewe ili wote waikose makoroboi.
Katika sekeseke hilo wamachinga zaidi ya 40 wamekamatwa kwa kukiuka sheria za mipango miji.















