Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifungua shina la Wakereketwa la Waendesha Bodaboda Wilayani namtumbo,Kinana aliwachangia vijana hao kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya benki,ili waweze kupata mikopo ya kununua piki piki kwa ajili ya shughuli zao.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wanancho hao walikwenda mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.Vita Kawawa amewatuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na Ofisa Ushirika wa mkoa huo wa kuwambambikizia madeni wakulima wa Tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea,ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na Wananchi kuachiwa mzigo mkubwa wa kulipa madeni ambayo hayawahusu,hali inayowapelekea wakulima hao kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.
Mbunge wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro Wialayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata chai nyumbani kwa balozi wa shina,Said Husein mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama na kukagua uhai wa chama katika mkoa wa Ruvuma
Ndugu Kinana na Ujumbe wakienda kukagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto,kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
