Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto)
akiwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na
kiongozi wa Taasisi ya Tanga Women Development Initiative (TAWODE)
wakizundua mradi huo.
Watoto
wa Kike wakifuatilia uzinduzi wa taasisi yao.
OKTOBA
11 ya kila mwaka ni siku ya mtoto wa kike duniani. Mkoani Tanga waliadhimisha
siku hiyo ya mtoto wa kike kwa kuzindua mradi maalum wa kuwajengea uwezo
wasichana wa mkoa wa Tanga chini ya Taasisi ya Tanga Women Development
Initiative (TAWODE).
Mgeni
rasmi katika uzinduzo huo uliofanyika uwanja wa michezo wa Mkwakwani alikuwa
Mhe Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, na kuhudhuriwa pia na Mbunge wa Viti
Maalum mkoa wa Tanga, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia
na Watoto, Ummy Mwalimu na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tanga wakiongozwa na
Halima Dendegu .
Akizungumzia
uzinduzi huo Naibu Waziri mwenye dhamana hiyo ya Jinsia, Ummy Mwalimu alisema
kuwa amefurahishwa sana na uzinduzi wa mradi huo.
“Kupitia
mradi huu ninafurahi kuona nikitekeleza kwa vitendo dhamira yangu kama kiongozi
- 'niliechaguliwa' na wanawake wa mkoa wa Tanga- kuchangia kuboresha maisha ya
Wanawake na Watoto wa Mkoa wa Tanga”, alisema Mwalimu.
Pia
shukrani zilienda kwa Balozi wa Denmark nchini, Johnny Flento kwa kuunga mkono
jitihada hizo.
Mradi
huo utatekelezwa ktk Wilaya za Pangani, Muheza, Mkinga, Lushoto na Tanga Mjini,
umelenga kuchochea uwezo na ubora wa wasichana (wa umri wa miaka 10-24),
kutambua weledi na umuhimu wao kwa maendeleo yao na ya jamii zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa alisema kuwa kupitia mradi huo Mkoa umedhamiria
kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wasichana waliopo katika shule za Serikali za
Msingi na Sekondari, kuboresha hali ya afya ya uzazi, kupunguza mimba za
mapema, ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU.
“Tumepanga
kuwafikia moja kwa moja wasichana 16,000 na zaidi ya 100,000 kupitia njia
mbalimbali ikiwemo mabango, Radio jingles (Mwambao FM 106.0), matamasha ya
wasichana na njia nyingine mbalimbali,”alisema Galawa.
Aidha
Wasichana 1,000 waliopo shuleni na wanaoishi ktk mazingira magumu wataingizwa
katika Mfuko wa Bima ya afya ili kuweza kupata huduma za afya bure.
Endapo
jitihada hizo zitazaa matunda zitachochea maendeleo ya wanaTanga ambao wamekuwa
na utayari wa kupokea ushauri na mawazo ya wadau mbalimbali juu ya
Utekelezaji mzuri wa Mradi huo.



