Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman
Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni
mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania
(RTD).Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma
Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa
lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili
wa Marehemu Julius
Nyaisangah.
Mkuu
wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu
Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali
mbali hapa nchini wakishirikiana kwa pamoja kubeba Jeneza lenye Mwili wa
Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J) ulipowasili kwenye Viwanja vya Leaders
Club,jijini Dar es Salaam leo.






