Shughuli ya Upasuaji
mgonjwa wa Moyo ikiendelea.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwajulia
hali baadhi ya wagonjwa kati ya watoto 18 waliokwishafanyiwa upasuaji
katika Hospitali ya Bugando kwa gharama ya SH. 50, 000/ badala ya gharama
sahihi ya Sh. milioni 6. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, leo amehudhuria
Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini
hapo na kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za
Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu
kushoto) akishuhudia zoezi la upasuaji wa Moyo alipokuwa akifanyiwa mmoja
wa wagonjwa wa Moyo ndani ya Hospitali ya Bugando, baada ya kuzindua Jengo
la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani
Mwanza leo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando,
iliyofanyika leo Hospitalini hapo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwahutubia wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando, wakati wa sherehe
za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando 'Bungado Day', iliyofanyika leo
jijini Mwanza sambamba na uzinduzi wa Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa
saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia
moja kati ya chupa ya mafuta ya Vaseline, ambayo ni 'Feki' yaliyokamatwa
na TFDA, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye
Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo sambamba na
uzinduzi wa Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji
wa Moyo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa
Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo, katika Hospitali ya Bugando Mkoa
wa Mwanza, wakati wa wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando,
iliyofanyika leo Hospitalini hapo.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
