Oct 13, 2013

...BREAKING NEWSSSSSS!!!! MWANDISHI WA HABARI WA ITV&RADIO ONE UFOO SARO AMEPIGWA RISASI HUKU MAMA YAKE MZAZI NAYE AKIPIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.

ufoo saro


Taarifa za kusikitisha ambazo tumezipata hivi punde zinasema mtu mmoja
anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio
One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na yeye mwenyewe kujiua.
akizungumza na mtandao huu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa
kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya
alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi umoja wa
mataifa UN huko sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo
gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado
hazijathibitishwa)
Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili
hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama
mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama
mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama
yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga
Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani
kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya
kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.