Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump
Kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Donald Trump kutoka katika miji mbalimbali nchini Marekani.
Maelfu ya raia kwa sasa wamekusanyika
nje ya mnara maarufu kama Trump Tower mjini New york wakipaza sauti zao
kuhusu sera za uhamiaji,mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi
yanayopingwa na Donald Trump.
Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wa urais.