Oct 31, 2016

NEWZ ALERT;BONDIA THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA

Taarifa iliyoifikia  asubuhi hii, inaeleza kuwa Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na mwili wake kukutwa maeneo ya Tabata, Jijini Dar es salaam. akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamasumbwi huyo, Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) amesema Mashali amefikwa na umauti huo usiku wa kumkia leo kwa kudaiwa kupigwa mpaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi. tutaendelea kujuzana taarifa zaidi za msiba huu wa Mwanamasumbwi huyu nguli hapa nchini, endelea kutembelea Libeneke la Globu ya Jamii.