
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akitizama vitabu wakati akitembelea katika sehemu za maonyesho zilizoandaliwa kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akitizama moja ya maonyesho ya mafunzo yanayotolela kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo akizungumza katika semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka CHAHITA kwenye semina ya ufunguzi wa mafunzo ya hisabati kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma,ya kuandikishia watoto kwaajili ya kupata vipimo wakati akifanya ukaguzi wa huduma katika Kituo cha Afya cha Makole katika Manispaa ya mkoa wa Dodoma.
Na Nasra Mwangamilo
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo akiwa katika sehemu ya kuandikishia watoto
kwaajili ya kupata vipimo wakati akifanya ukaguzi wa huduma katika Kituo cha
Afya cha Makole katika Manispaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri aliyasema hayo wakati akitoa hotuba katika ufunguzi wa semina
ya mafunzo ya hesabu iliyoandaliwa na chama hicho itakayoendelea kwa muda wa
siku sita katika moja ya majengo ya ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma .
“Nimefarijika sana kwa ninyi kunipa fursa kuwa nanyi
katika siku ya leo kwani najua lengo kubwa la semina yenu lakini pia lengo kubwa la chama chenu ni
kuhakikisha taaluma ya hesabu inatamalaki katika nchi yetu ikiwa lengo kubwa ni
kupata wataalamu wazuri waliobobea katika Nyanja hii”alisema Mh. Jafo.
Mh. Jafo aliongeza kuwa kwa sasa ni muhimu kufanya
tathmini ni kwa namna gani wanaweza kuhakikisha ufaulu wa hesabu unaongezeka
kwa wataalamu kuweza kubuni mbinu
tofautitofauti za ufundishaji wa somo hilo na kuhakikisha mbinu hizo
zinatawanyika katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa
katika kulisoma somo hilo.
Akiongea kwa niaba ya CHAHITA mwenyekiti wa chama hicho
Dk. Said Sima alieleza malengo ya chama hicho kuwa ni kuwaendeleza na kuwapa mafunzo walimu katika vijiji 489 na wilaya zote
nchini ili kuhakikisha wanafundisha wanafunzi somo la hisabati kwa dhana ya
nadharia na vitendo.
Pia Dk. Sima alitoa
mapendekezo kwa Mh. Naibu Waziri ambayo
ni kuongezewa malipo kwa walimu wa somo la hesabu, Serikali kubuni mpango kwa
wanafunzi wa elimu ya juu ya ualimu wa somo la hesabu kuwa wanasaidia
kufundisha katika shule za jirani na vyuo wanavyosoma na kubuni mpango wa
walimu wa somo hilo kuwa wanapewa muda wa ziada wa kuwafundisha wanafunzi.
Chama hicho ambacho kwa sasa kina miaka 51 tangukilipo
anzishwa tarehe 11 ya mwezi wa kwanza mwak 1966 kimeanza semina hiyo leo
ikiwajumuisha walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka ndani nan je ya
Dodoma, Walimu kutoka Vyuo vikuu, Wawakilishi kutoka NACTE na NECTA na wawakiliski kutoka Chama cha
Walimu Tanzania (CWT).