Wachimba migodi haramu waliokuwa wamekwama chini ya ardhi kwenye
mgodi mmoja nchini Afrika Kusini tangu siku ya Jumatano wameokolewa.
Polisi
wanasema kuwa wanaume hao watatu walibuka kutoa ardhini mapema leo
wakiwa wamejawa na vumbi, na kisha kutoroka wakihofia kukamatwa kwa
kuendesha shughuli haramu.
Ripoti zaidi zinasema kuwa juhudi za uokoaji zimesitishwa kutokana na
kuwepo moto chini ya ardhi, lakini jamaa za wachimba migodi waliokwama
wanataka shughuli hiyo kuendelea.
Maelfu ya wachimba migodi wasio na vibali hufanya kazi kwenye migodi mingi ya dhahabu, maeneo yanayozunguka mji wa Johannesburg.

