Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa
mkopo ajira badala lake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na
akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa
aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia mtandao wa
Facebook.com/eatv.tv.
“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote
asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni
kuwawezesha kupata elimu basi” – Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa amesema pia wanufaika
wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la
mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa
kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza
kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu
ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri
majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo
walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.
– EATV