
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wafanyabishara na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali hapa nchini kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Alikutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016.
Baadhi ya Mabalozi na Wafanyabiashara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao , Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam Septeba 13, 2016 kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati Miundombinu ilitoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kageza. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na Sheila Simba, MAELEZO
Jumla
ya shilingi bilioni 1.4 zimechangwa na mabalozi na wafanyabiashara kwa
ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani
Kagera.
Michango
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam katika harambee iliyoongozwa na
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kufanyika Ikulu. Akizungumza
katika harambee hiyo Waziri Mkuu alisema jumla ya nyumba 840 zimebomoka
na kuharibika kabisa, wakati nyumba 1264 zimepata hitilafu na zinaweza
kufanyiwa marekebisho ili watu waendelee kuishi katika nyumba hizo.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa shule 4 za sekondari ambazo ni Nyakato, Ihungo,
Kashange na Buhembe zimeharibika na mbili kati ya hizo yaani Ihungo na
Nyakato zimefungwa kutokana na kuharibika sana.
Madhara
mengine yaliyosababishwa na tetemeko hilo kwa mujibu wa Waziri Mkuu ni
kuharibika kwa vituo vya afya, miundombinu ya barabara, umeme na njia za
mawasiliano na kufanya athari za tetemeko kuwa kubwa.
Kutokana
na athari hizo Waziri Mkuu amewaomba mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao
hapa nchini kusaidia waathirika kwani ni tukio ambalo halikutarajiwa na
limeleta hasara kubwa kwa wanakagera na Taifa kwa ujumla. “Licha
ya michango hii ninayowaomba leo, tutaandaa safari kwa anayehitaji
kwenda kujionea hali halisi ili aone ni namna gani
atakavyosaidia,”alisema Waziri Mkuu.
Aidha,
Mhe. Majaliwa amesema kuwa imefunguliwa akaunti ya kuchangia katika
maafa hayo kwenye benki ya CRDB inayojulikana kama KAMATI MAAFA KAGERA
akaunti namba 0152225617300 na swift code ambayo ni CORUtztz na kuwaomba
wananchi na watu wengine kutumia akaunti hiyo kwa kusudi hilo. Majaliwa
amesema pia kuwa utaratibu unaandaliwa ili kuwawezesha watu kuchangia
kwa njia ya Mpesa, tigopesa na Airtelmoney. Utaratibu huo utakapokuwa
tayari utatangazwa ili kuwarahisishia watumiaji wa mitandao hiyo
kuchangia.
Katika
harambee hiyo wafanyabiashara waliochangia ni Mwenyeki Mtendaji wa
kampuni za IPP Dkt Reginald Mengi aliyechangia Tsh million 110, Mohamed
Dewji ametoa milioni 100, Subash Patel milioni 150 na Salim Turki
aliyetoa mifuko 5000 ya saruji na mabati 3000.
Wengine
waliochangia ni kampuni mbali mbali zikiwemo kampuni ya bia ya
Serengeti iliyotoa mifuko 800 ya saruji, Sahara Tanzania wametoa
shilingi milioni 20, Camel Oil kupitia Camel Cement wametoa mifuko 1000
ya saruji ,Puma wamechangia shilingi million 50, Pepsi Cola wametoa
milioni 50 na Azania Group wamechangia milioni 50.
Baadhi
ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini waliochangia ni pamoja
na ubalozi wa China shilingi milioni 100 na kupeleka
madaktari,dawa,mahema na vifaa vingine kwa ajili ya kusaidia waliopatwa
na maafa hayo. Kuwait
kupita ubalozi wao nchini wamechangi dola elfu 10 za Kimarekani na euro
elfu 10, na Nchi ya Kenya iliyopeleka msaada wa mahema,magodoro na
dawa.
Wizara
ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wametoa milioni 10,
mwakilishi wa China Merchantile Group ametoa milioni 100, Toyota
Tanzania milioni 10, Kamal Group milioni 50, Urban Group milioni 20, TBL
milioni 100, IPTL 50, Tanzania Agriculturak Processing Zone milioni 30,
Umoja wa wafanya biashara ya mafuta ya rejereja milioni 250 na Group
Six wametoa tani 80 za saruji.
Wengine
waliochangia ni pamoja Jambo plastic milioni 20, Tanga Cement mifuko
1000 ya saruji, Agusta Tz milioni 10, Oryx milioni 50, Kagera Sugar
milioni 100 na tani 10 za sukari, Tipper milioni 20 ambapo GBP, Oilcom
na Moil watajenga shule mbili zilizoharibika.
Uchangiaji
huo umejumuisha pia na watu binafsi ambao ni wakili wa kujitegemea,
Bwana Protase Ishengoma milioni 5 na Melisa Kataraiya milioni 20.
Tetemeko
hilo la ardhi ni kubwa kuliko yote ambayo yamewahi kutokea hapa nchini
na hadi sasa limesababisha vifo vya watu 17 na kuharibu nyumba, majengo
na miundombinu mkoani Kagera.
chanzo: michuzi media