
Meneja
Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie Massawe(Wapili kutoka Kulia)
akiwa na wafanyakazi wa Tanga Simenti wakionesha mfuko wa Simenti wa
Kilo 50 wakati wa uzinduzi na kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. 

Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati
wa kuitambulisha bidhaa mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini
Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa
Tanga Simenti, Mtanga Noor


Baadhi
ya wafanyakazi wa Tana Simenti wakiwa kwenye mkutano wa kuitambulisha
Simenti mpya ya Mkombozi- simenti ya mwendokasi jijini Dar es Salaam
leo.

Meneja
wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe.
SIMENTI Public Limited Company (TCPLC) wazalishaji wa simenti hapa nchini wamezindua bidhaa bora ya simenti inayoitwa, MKOMBOZI.
“Bidhaa
hii mpya ya Tanga Cement ni hatua nyingine ya kuwa karibu na Watanzania
kwa kubuni na kuwaletea aina nyingine ya simenti, ambayo mbali na kuwa
ni ya bei ya kuridhisha kwa Mtanzania wa kawaida bado inawahakikishia
ubora dhabiti unaoendana na teknolojia ya kiwango cha juu katika
utengenezaji wa simenti”.
Ameyasema
hayo wakati wa kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya
Mwendo Kasi, Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie jijini Dar es
Salaam leo.
Amesema
kuwa mahitaji ya wananchi ni makubwa kukabiliana na ongezeko la miradi
ya miundombinu na wakati huo huo mahitaji ya simenti bora katika ujenzi
miundombinu na nyumba za makazi katika maeneo ya mijini na hasa vijijini
ambapo utaalamu katika ujenzi.
Bidhaa
mpya ya simenti ya MKOMBOZI – ‘simenti ya Mwendokasi' inaletwa kwa
Watanzania ili kuharakisha maendeleo ya makazi bora na shughuli nyingine
za ujenzi kama jina linavyojieleza.
MKOMBOZI,
simenti ya daraja la nguvu kwa kiwango cha 32.5 N, ni simenti ambayo
bei yake ni ya kuridhisha ambapo mtu yeyote anayehitaji simenti kwa
ujenzi wa aina yoyote anaweza kununua.
Mkombozi
imekuja kuwapatia watanzania kile wanachohitaji katika ujenzi wa
miundombinu pamoja na makazi hii ni simenti kwa matumizi yote, simenti
kwa aina zote za ujenzi.