
Kutoka
kushoto, Grace Kijo- Mratibu wa Masoko wa Etihad nchini Tanzania na
Balozi wa Korea nchini Tanzania, Song Geum –Young, wakimpongeza Bi.
Heejin Hwang (kulia) kwa kushinda moja ya tiketi tatu za safari ya
Korea. Washindi wengine wawili katika sherehe hiyo iliyofanyika jijini
Dar es Salaam ni YoungMi Choi na Sunmi Oh

.Kutoka
kushoto; Grace Kijo, Balozi wa Korea na Bi. HaeMyung Rhee, Mwenyekiti
wa Chama cha Korea, wakimpongeza Bi. Heejin Hwang. kwa kushinda moja ya
tiketi tatu za safari ya Korea. Washindi wengine wawili katika sherehe
hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ni YoungMi Choi na Sunmi Oh.

Grace Kijo akipokea tuzo ya kutambua mchango wa Shirika hilo kwa niaba ya Etihad.
SHIRIKA
la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake Nchi za Falme za Kiarabu
limeungana na Jumuiya ya Wakorea waishio nchini Tanzania kuadhimisha
sherehe ya kitamaduni ya taifa hilo inayofahamika kama ‘CHUSEOK’ kwa
kutoa tiketi kwa safari watatu kutoka Dar es Salaam kwenda Incheon-South
Korea.
Akizungumza
katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Wakorea wanaoishi
hapa nchini, Bi. Hae Myung Rhee alilishukuru Shirika la Ndege la Etihad
kwa udhamini wake kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa
na wadau muhimu pamoja na wafanyabiashara na wanachama takribani 250 wa
jamii ya Kikorea hapa Tanzania.