Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua
kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani
ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa.
Itakumbukwa hivi karibuni CUF
kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya
mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.
Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na
waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar
es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar