
Ndege mpya ya
kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya
Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa
heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake
(Water Salute).
Baada ya kupokea
heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).Akizungumza baada
ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema
ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya
kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe
itakayotangazwa baadaye.