Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura
akiangalia baadhi ya kazi za Sanaa kutoka kwa Wasanii wakati wa uzinduzi
wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la
Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel Production
lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura
akimkabidhi Cheti cha ushiriki Bw.Adrian Nyangamale Rais wa Shirikisho la
Sanaa za Ufundi katika uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Msanii Duniani
lilioandaliwa na Baraza laTaifa la Sanaa (BASATA)pamoja na Kampuni ya Haak Neel
Production lililofanyika Septemba 24 Jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura ametoa
agizo kwa wasanii nchini kuhakikisha wanasajili kazi zao katika Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) ili watambulike kwa mujibu wa Sheria.
Agizo
hilo amelitoa jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Tamasha la
Siku ya Msanii Duniani lilioandaliwa na Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA)
ambapo amewaahidi wasanii kuwa wakijisajili watatambulika na itakuwa
rahisi kwa Serikali kujua changamoto wanazozipata na kuzitatua kwa urahisi.
“Napenda
mtambue kwamba suala la Urasimishaji linakwenda sambamba na uwepo wa Haki
Miliki ya kazi za ubunifu, nawashauri mtunze Haki Miliki zenu na msiziuze na
wale wabunifu wapya na ambao hamjasajili kazi zenu nawaomba mfanye hivyo
ili kuepuka uharamia”.Alisisitiza Mhe. Anastazia.
Aidha
Mhe.Naibu Waziri amewaomba wadau wote wa Sanaa kutoa maoni yao katika kuboresha
tasnia hii yenye kubeba maeneo kama Muziki, Filamu, Maonyesho, Ususi, na
Uchoraji ili kuwezesha tasnia hii kujulikana na kuboresha mapato ya
Wasanii.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey
Muingereza amewataka Wasanii kutunza vibali wanavyopatiwa na Baraza hilo
kwani ndio utambulisho wao popote wanapokuwa na inakuwa rahisi wao kusaidiwa
wanapopata changamoto.
“Wengi
wenu mmejisajili lakini wale wachache ambao bado naomba mfanye hivyo ili sisi
tuwatambue na Sheria ya Haki Miliki pia iwatambue”.Aliongeza
Bw.Muingereza.
Naye
Msanii wa Uchongaji Bibi Hapiness Mmbaga amewashauri wanawake kupenda fani hiyo
na kuacha dhana inayosema kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu kwani
ulimwengu wa sasa umebadilika hakuna tena kuchagua aina ya kazi ya kufanya.
Tamasha
la siku ya Msanii duniani linaadhimishwa kwa mara tatu mfululizo ambalo
linalenga kuthamini mchango wa kazi za Sanaa hapa nchini ambao kauli mbiu yake
ni “Nguvu ya Sanaa”na kilele chake itakuwa ni tarehe 26 mwezi oktoba
mwaka huu.