Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya oparesheni ambazo zimefanyika
maeneo mbalimbali na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. ambapo
Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja kwa tuhuhuma za
ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionesha
kwa wanahabari silaha zilizokamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro
akionyesha gari aina ya Verosa likiwa limesheheni magunia saba za bangi
leo iliyokamatwa hivi karibuni jiji Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha gari aina ya Noah ikiwa wan a magunia ya bangi.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha namba za gari za bandia ambazo zimekuwa zikitumiwa na
waharifu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya
jamii.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu wawili
ambao ni Mme na Mke kwa tuhuma za matukio mbalimbali ya ujambazi wa
kutumia silaha za moto katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es
salaam.
Watuhumiwa
hao ambao wametambulika kwa majina ya Bakari Abdallah (40) na Sihaba
Omary (28) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni walitiwa mbaroni mnamo tarehe
23 Septemba mwaka huu na Kikosi Maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na
ujambazi wa kutumia silaha.
Akizungumza
mbele ya wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam,
Kamishna Simon Sirro, alisema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba mwaka huu
Askari walifika nyumbani kwa watuhumiwa hao na kukuta bastola aina ya
"BROWNING" yenye usajili namba CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na
risasi tano pamoja na simu aina ya Nokia Lumia ambayo inadaiwa kuwa
iliporwa katika matukio ya unyang'anyi.
Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.