Mjumbe kutoka ubalozi wa China nchini Gou Huodong,akielelezea jinsi atakavyowahamasisha wawekezaji wengi kutoka China waje kuwekeza Mkoani Arusha,pembeni ni Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akipeana mkono kama ishara ya ushirikiano baina ya nchi ya China na Mkoa wa Arusha na Mjumbe kutoka ubalozi wa China Nchini Gou Huodong.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe kutoka nchini China na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake.
Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingiza mazuri na usalama kwa wawekezaji kutoka China watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.
Kutoka
ubalozi wa China kwa Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia
Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda kuwahamasisha wachina wengine
waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha hasa kwenye sekta ya
Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza pato la taifa
kwa asilimia kubwa.“Nitaenda kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa
wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa
ya Utalii kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.