Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mpinduzi (UVCCM) mkoani Arusha amezuiwa
kuingia ofisini leo asubuhi na baadhi ya makada wa chama hicho kufuatia
tuhuma zinazomkabili za kughushi nyaraka za Usalama wa Taifa na
kufanyia utapeli.
Makada wa chama hicho walifunga ofisi hizo mapema leo alfajiri
wakisema kuwa mwenyekiti huyo, Lengai Ole Sabaya hana hadhi tena ya kuwa
mwenyekiti wa umoja huo mkoani Arusha baada ya kughushi nyaraka za
Idara ya Usalama wa Taifa kufanya utapeli.
Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa UVCCM Arusha.
Baadhi ya makada ambao ni watiifu kwa mwenyekiti huyo wameonekana
wakimsaidia aweze kuingia ofisini wakijitahidi kuwaondoa waliokuwa
wakimzuia bila mafanikio.
Tazama video hapa chini ya mvutano ulivyokuwa.

