Katika
uteuzi ulifanywa mwezi Julai na Rais Magufuli wa wakurugenzi wa
Halmashauri mbali mbali za miji na wilaya, ambao ulitangazwa na Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe, kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65
waliteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 walikua
wakurugenzi wapya kabisa. Kati yao Wakurugenzi 13 hawakuripoti kabisa
katika vitengo vyao vya kazi kwa sababu tofauti tofauti kama kuwepo
masomoni, kupatwa na ugonjwa au hali ya kiafya kutokumruhusu kushika
wadhifa wowote na wengine kutokua na sifa za kitaaluma hivyo kushindwa
kukidhi vigezo vya kuendelea kuwepo kwenye nafasi hizo.
Licha ya Serikali kushindwa kuyataja
majina ya Wakurugenzi ambao hawakuripoti katika vituo vyao vya kazi au
kutoa sababu za wao kushindwa kuripoti kazini, Tumeweza kufanya
uchunguzi na kugundua Wakurugenzi waliteuliwa mwezi Julai ambao
hawatashika nyazifa hizo kutokana na Rais kuteua Wakurugenzi wengine
kushika wadhifa huo siku ya tarehe 10 mwezi Septemba.
Majina ya wakurugenzi 13 ambao hawatashika nafasi zao hizo kutokana na sababu zisizojulikana:
Bagamoyo DC – Azimina A. MbilinyiMkalama DC – Martin Msuha Mtanda
Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko
Moshi DC – Emalieza Sekwao Chilemeji
Kibondo DC – Shelembi Felician Manolo
Nachingwea DC – Bakari Mohamed Bakari
Ulanga DC – Audax Christian Rukonge
Nsimbo DC – Joachim Jimmy Nchunda
Mbulu DC – Festi Fungameza Fwema
Ukerewe DC – Tumaini Sekwa Shija
Bukoba DC – Abdulaaziz Jaad Hussein
Tarime Mji – Hidaya Adam Usanga
Dodoma Manispaa – Dkt. Leonard M. Masale
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima, Toleo namba 4304, Septemba 15,2016
chanzo: swahili times