WATU
15 wamepoteza maisha nchini Bangladesh baada ya moto mkubwa
uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji katika kiwanda
kimoja.

Zaidi
ya watu 70 wamejeruhiwa kwenye tukio hilo lililotokea pembeni mwa Mji
Mkuu wa nchi hiyo, Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga
dunia ikaongezeka zaidi.
Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100
walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo
ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne