Katikati
- Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampeni ya Declutter and Donate Bi.
Nasra Karl akiongea na waandishi wa habari katika mkutano jijini Dar es
Salaam (kushoto) Hyacinta Ntuyeko - Mkurugenzi wa Glory Sanitary Pads
(Kulia) Aunty Sadaka - Lifestyle Consultant na kushoto kabisa Bi Stella
Malisha - Mkurugenzi wa IS Duke International.
Aunty
sadaka akitilia mkazo umuhimu wa kampeni ya declutter and donate kwa
waTanzania wote. Kushoto kwake ni Bi. Stella Mashila Mkurugenzi wa IS
Duke International.
Bi
Hyacinta Ntuyeko wa Glory Sanitary Pads akijibu swali kutoka mwandishi
wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Declutter and Donate
iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Bi Nasra karl Mwanzilishi
na Mkurugenzi ya kampeni ya Declutter and Donate na pembeni yake Aunty
Sadaka Lifestyle consultant.
Bi
Nasra Karl, Mkurugenzi na Mwanzilishi ya kampeni wa Declutter and
Donate akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI
ya Elite Organizing Services Limited imezindua kampeni inayoitwa
Declutter and Donate jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa
kampeni ya aina hii kuzinduliwa nchini Tanzania. Kampeni ya Declutter
& Donate ni mpango wa kijamii unaohamasisha umma kugawa vitu
ambavyo hawavihitaji.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa kampeni Bi Nasra Karl alisema “wazo la kuanzisha
kampeni hii lilikuja hapo mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli
alivyotamka kuwa siku ya Uhuru itasherekewa kwa kufanya usafi ila
kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu. Hapo basi tulikuja na wazo yakuanza
kusaidia nyumba na biashara mbali mbali kuepukana na vitu wasiyo hitaji
ambayo inasaidia kukuza mazingira safi na kusaidia kuzingatia ubora
katika maisha yetu ya kila siku.
Kuwa
kampuni ya uandalizi inayotoa huduma kusaidia watu binafsi na biashara
mbali mbali kuepuka kuishi na vitu wasiyo viihitaji na maisha ambayo
yanampangilio, ELITE ORGANIZING SERVICES LIMITED iliona haja ya kuongeza
uelewa kuelimisha umma maana ya kutoa vitu visivyo na umuhimu katika
maisha yao ( declutter) na ni jinsi gani vinaweza kupunguzwa katika
maisha ya watu na jinsi gani inaweza kutumika kwa manufaa ya wengine.
Kama msemo maarufu ya kingereza inayosema ‘ Taka taka ya mwanaume moja
ni dhahabu kwa mwanaume mwingine’
Kampeni
ya Declutter & Donate Campaign itaanza mwezi wa tisa Septemba
na kuisha mwezi wa kumi na mbili yaani miezi mitatu.
Katika
kipindi hiki tunawaomba watu binafsi, familia na biashara mbali mbali
kugawa vitu vyao ambayo zimetumika na kuuuzwa katika yard sale, mwanzoni
mwa Disemba tunategemea kuwa na tukio itakayo changisha kwa ajili ya
kituo inayosaida watu. (charity).
Mwishoni
mwa Disemba tutakuwa na tukio ambapo tutakuwa na wataalamu wa
kudeclutter wakija kuongea na wa Tanzania na kuwaeleza jinsi ya
kuepeukana na vitu visivyo na muhimu katika biashara zao, nyumba zao na
maeneo yanayowazunguka.
Mwaka
huu kampeni ya Declutter & Donate watasaidia watoto yatima na
wanawake wanaoishi katika mazingira magumu. Mwaka huu tunapenda kusaidia
wanawake wanaopata shida katika usalama ya hedhi na ‘Mtoto anayesoma
atakuwa mtu anayeweza kufikiri’ kwa watoto wanao ishi katika mazingira
magumu.
Mara
nyingi tukietembelea watoto yatima na kugawa chakula, nguo na vitu
vingine vya kutumia kila siku tunasahau kwamba michezo na vitabu vina
jukumu kubwa katika ukuaji bora wa motto na ndio maana tumeamua kuwapa
michezo na vitabu.
Tunapokea
fenicha, vifaa vya nyumbani, vitabu vya watoto na michezo ya watoto.
Hivi sasa tunaishughulikia mahala pakuacha hiv vitu na tutaweza
kuwajulisha hivi karibuni kupitia vyombo vya habari