Mwanamuziki wa nyimbo za asili,
Jasmin a.k.a The African Lady anayewika na ngoma yake iitwayo Omunyamlo
akikamua kwenye shoo hiyo.
Mc wa Dar Live, Brighton a.k.a Daraka akiwa kwenye pozi na Topito
Mpiga picha: Issa Mnally/Boniphace Ngumije.
KUNDI la Muziki wa Taarab lisilo na mpinzani Bongo, Jahazi Modern
sambamba na Mfalme wa Singeli, Msaga Sumu jana waliandika historia ya
aina yake baada ya kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya Sikukuu
ya Idd el Hajj ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo
Mbagala-Zakhem jijini Dar.Katika shoo hiyo ambayo ilianza kufunguliwa na wasanii chipukizi wanaofanya vizuri kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva wakiwemo Lamuzika Vijana Classic, AD Classic, Tamaduni, Topito na MC wa Dar Live, Brighton Darada, Jahazi walipafomu ngoma zao zote kali zikiwemo Nipe Stara na Nilijua Nitasema.
Kwa upande wa mfalme wa muziki wa uswahilini, Msaga Sumu yeye pia alikamua ngoma zake zote kali bila kusahau Unanitega Shemeji, Mama wa Kambo na Chura.