Cyprian Okoro, 55, kutoka Kusini
Magharibi mwa London alipatikana na makosa matano ya kuwa na video za
ngono ya kuchukiza zaidi pamoja na picha moja ya utupu ya mtoto.
Mshtakiwa, ambaye anatoka Cameron Place,
Streatham, amekanusha mashtaka hayo na amepewa dhamana lakini
atahukumiwa tarehe 30 Septemba.
Mahakama iliambiwa kwamba Okoro alikuwa na picha na video hizo kwenye simu yake baada ya kuzipokea kupitia WhatsApp.
Ni mara ya pili kwa Okoro kupatikana na
hatia wakati mnamo mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 18
baada ya mwanamke kuwasilisha tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi
yake.
Okoro alihitimu kama daktari Lagos, Nigeria, mwaka 1986.