
Katibu
Mkuu Ban Ki Moon alipomkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dk. Augutine Mahiga ambaye anamwakilisha Rais John
Pombe Magufuli katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na ujumbe wake akiwa katika
Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameitaka Tanzania kuendelea na
kazi nzuri ya usuluhishi wa migogoro katika baadhi ya nchi za Maziwa
Makuu.Ban Ki Moon ametoa wito huo jana ( jumatano) wakati alipokutana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Augustine
Mahiga, ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea hapa
Jijini New York, Marekani.Katika mazungumzo hayo Mkuu huyo wa Umoja wa
Mataifa amesema, Tanzania ni kutovu cha Amani, usalama na demokrasia, na
kutokana na sifa hizo Tanzania, inapashwa kuendelea na juhudi zake za
kuzisaidia nchi zenye migogoro.
Akazitaja
nchi hizo kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi na Sudani ya
Kusini ambayo ameitaja kuwa ipo katika kipindi kigumu sana.
“
Ninawashukuru sana viongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri ya
utafutaji wa Amani katika nchi zenye matatizo, Sudani ya Kusini ni nchi
ambayo inatupa mashaka makubwa. Rais asaidie katika kurejesha hali ya
utulivu.Tanzania ni nchi kubwa kwa hiyo bado ninaendelea kuitumainia.”
akasisitiza Ban Ki Moon.Vile vile Katibu Mkuu Ban Ki Moon ametoa pia
shukrani wa ushiriki wa Tanzania katika operesheni za ulinzi wa Amani na
kazi na weledi mkubwa unaoonyeshwa na wanajeshi wa Tanzania.
Akatumia
fursa hii kuishukuru Tanzania na viongozi wake kwa mchango wao mkubwa
uliofanikisha yeye kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Na
akatoa pole zake kwa serikali na kwa watanzania baada ya kupata taarifa
kuhusu tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na uharibifu wa mali.
“Naishukuru
sana Tanzania, namshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kiwete na wewe ( Waziri)
na viongozi wengine, mlichangia sana kwangu mimi kuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa. Ninawashukuru sana sana. ” .Katibu Mkuu Ban Ki Moon
anamaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka kumi mwishoni wa Mwaka
huu.Na tayari mchakato wa upigaji kura wakumtafuta mrithi wake
unaendelea katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Kwa
upande wake, akiwasilisha salamau za Rais John Pombe Magufuli, Waziri
Mahiga amesema. “ Ninawasilisha salamu za Mhe. Rais, alipenda sana
kuhudhuria mkutano huu wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa
bahati mbaya ilimbidi kuahirisha safari yake kutokana na tetemeko la
ardhi lililotokea hivi karibu nchini kwetu ”.
Ban
Ki Moon akimkabidhi kitabu Waziri Mahiga, kitambua ambacho Mkuu huyo wa
Umoja wa Mataifa anasema kimeandika na kuelezea utekelezaji wa majukumu
yake na kwamba ni kitabu kizuri kutumika kama hadidu ya rejea
Aidha
Waziri Mahinga ametumia pia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Katibu
Mkuu kwa utekelezaji wa kutukuka wa majukumu yake katika kipindi cha
miaka kumi ya uongozi wake.
“Kwa
niaba ya serikali ya Tanzania nikupongeza kwa utekeleaji wa majukumu
yake. Ulionyesha ushirikiano wa karibu na Tanzania, ushirikiano
uliokuwezesha kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu na
msaidizi wako wa karibu. Lakini pia uliniteua mimi kuwa Mjumbe wako
Maalum huko Somalia . Tanzania inashukuru kwa haya na mengine” akasema
Mahiga.
Aidha
amemwelezea Katibu Mkuu kama kiongozi ambaye aliifanya Afrika kuwa
kipaumbele chake, lakini pia aliibeba sana ajenda ya wanawake jambo
ambalo amesema limemjenga sifa kubwa.Akizungumzia
kuhusu Tanzania kuendelea na juhudi za usuluhishi wa migogoro. Waziri
amemhakikisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, Tanzania na
viongozi wake wataendelea na kujukumu hilo.
“Ni
kuhakikishie kwamba Serikali yangu itendelea na jukumu hili la
usuluhisi. Na kwa upande wa Burundi Tanzania, inaushukuru Umoja wa
Mataifa, kwa kutambua na kuamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki
inaweza kuushughulikia mgogoro huu. Tanzania ambayo imekabidhiwa jukumu
la uwezeshaji wa mazungumzo ya Amani inataka kufanya kazi kwa karibu na
Umoja wa Mataifa hivyo misaada ya hali na mali kutoka Idara za Umoja wa
Matifa ni jambo muhimu”.Amesisitiza Waziri Mahiga

