Baada
ya muongozaji wa video nchini Hanscana kujitoa kwenye kampuni iliyokuwa
ikimsamimia,Wanene Entertainment,kwa upande wao (Wanene) wamefunguka na
kusema kuwa hakuna ugomvi kati yao na Hanscana bali tu walishindwa
kukubaliana kwenye vitu kadhaa.
Akiongea
kwenye mahojiano na radio 5,Gentriez ambaye ni mmoja kati ya watu wa
ndani wa kampuni hiyo amesema kuwa Hanscanah alisema anataka atimiziwe
vitu kadhaa la sivyo angevunja mkataba na ndichi kilichotokea.
“Ni
kweli Hanscana hayupo wanene Entertainment,hajafukuzwa lakini
amejiuzulu kutokana na mkataba aliopewa na kampuni hakuwa
ameuridhia.Yeye alitaka mahitaji fulani kwa kampuni kama Red camera,ili
afanye kazi kwa ufanisi zaidi,lakini kampuni ilimwambia asubiri kidogo
atumie zilizopo halafu mbeleni atapata hiyo camera maana ni hela ndefu
kidogo,pia alikuwa analalamika kuwa kampuni imewekeza hela nyingi kwenye
audio kuliko video,n hivyo tu hakuna bifu yoyote” alieleza Gentriez
CHANZO BOFYA HAPA