Waandishi wakimsikiliza Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia leo Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari hawapo
pichani juu ya vyama vinne vyenye uwakilishi bungeni vitarejea bunge
lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili
sintofahamu kwa vyama hivyo katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu
ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar,
Said Issa Mohamed akizungumza na waandishi habari juu ya maazimio ya
viongozi wa dini jana katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya
chama NCCR -MAGEUZI.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
VYAMA
vinne vyenye uwakilishi bungeni vimesema kuwa watarejea bunge lijalo
kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu
kwa vyama hivyo.
Akizungumza
na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
NCCR-MAGEUZI, James Mbatia amesema viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa
katika majadiliano hayo kwa kuweka masilahi mapana ya taifa.
Amesema
kuwa kurudi katika bunge lijalo mpaka wabunge wote wa vyama wakutane na
kuweza kufikia mwafaka huo kutokana na ushauri wa viongozi hao.
Mbatia
amesema kuwa kuna vitu vingine huwezi kuangalia katika katiba huvyo
unahitaji busara zaidi kwa kuangalia masilahi mpana ya taifa.
Amesema
kuwa NaibuSpika , Dk.Tulia Ackson anatakiwa kuweka busara katika
kuongoza bunge na kuacha taratibu kanuni za bunge pamoja na katiba.
Aidha amesema kuwa viongozi wa dini wameshauri vyama kurejea bungeni na kutaka masuala yao wanayoyataka kikatiba yatatuliwe.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii