Serikali ya
Zambia imeahirisha sherehe za kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Edgar
Lungu hadi wakati mwingine baada ya chama kikuu cha upinzani cha
Muungano wa Ustawi na Kitaifa (UPND) kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais
uliofanyika hivi karibuni nchini humo.
Chama cha UPND jana Jumamosi
kiliwasilisha mashtaka mahakamani kikitaka kuhesabiwa tena kura zote za
uchaguzi huo, suala ambalo limeilazimisha serikali ya nchi hiyo
kuahirisha zoezi la kuapishwa rais mteule.
Sheria za Zambia zinasisitiza kuwa,
iwapo chama chochote kitawasilisha mashtaka mahakamani kupinga matokeo
ya uchaguzi, rais mteule hawezi kuanza kazi rasmi.
Matokeo ya uchunguzi na uhakiki wa kura za uchaguzi wa rais wa Zambia yatatangazwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho
yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia, Rais Edgar Lungu wa chama
tawala cha Patriotic Front (PF) alishinda uchaguzi huo kwa kujinyakulia
asilimia 50.35 ya kura dhidi ya mpinzani wake, Hakainde Hichilema wa
chama cha upinzani cha UPND aliyepata asilimia 47.63 ya kura zote. Lungu
amemshinda mpinzani wake Hichilema ambaye ni mfanyabiashara tajiri kwa
tofauti ya takribani kura laki mbili