
Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki,
84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum
baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.
Kiongozi huyo wa zamani aliugua
akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi
jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.
"Aliandamana
na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya
watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na
familia yake ilisema.
Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada
ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa
Uingereza kwa matibabu.
Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu