(Kutoka
kulia) Mkurugenzi wa Stra8up Vibes, Sniper Mantana ambao ni waandaaji
wa Tamasha la “Monte Carlo Classic’ akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo) pichani wakati wa kumtambulisha Msanii maarufu kutoka Nigeria
Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama ‘Kiss Daniel’atakayepamba
uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi
ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.
Pamoja nae ni Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera, Msanii
kutoka Nigeria Kiss Daniel, mbia wa Tamasha hilo kutoka Malaysia
DeJurist Global na Meneja wa Msanii huyo Louiza Williams.
Meneja
Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akizunguzmza katika mkutano na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumtambulisha Msanii
kutoka Nigeria Kiss Daniel atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte
Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika
jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya
Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa
mara ya kwanza nchini Tanzania.
Mmoja
wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist
Global kutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel
ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo
litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la
Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni
Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays,
Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper
Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo
limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Msanii
maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama
Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake
katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika
ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar
es salaam.
Msanii
maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama
Kiss Daniel akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe
Bendera (kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana
(katikati) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa
kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini
la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi
uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mwanamuziki
maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina
la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao cha ‘Woju’ kwenye anga
za muziki, ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Monte
Carlo Classic tukio lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na
DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.
Mwimbaji
huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao
chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa tukio hilo Jumamosi hii jijini
Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee
Towers, Mtaa wa Ohio.
Akizungumza
mapema hii leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi
Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya
waandishi kwamba maandalizi ya tukio hilo yamekamilika na kuwasihi
Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
Aliongeza
kwamba kabla ya tukio hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na
itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.
Alisema tukio la the Monte Carlo Classic limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burdani.
“Kwenye
miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu
maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo
sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es
Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu,
huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye
hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.
Nae
Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki
hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo
limeifanya kuisogeza karibu na jamii benki hiyo. Tunayofuraha kuwa
sehemu ya uzinduzi wa tukio hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha
kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.
"Tukio
hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na
kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo
maeneo mbalimbali nchini.
Mwezi
uliopita Benki ya Bacrays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa
Kadi Bora za Visa nchini Tanzania. Kubeba fedha taslimu kuna kiwango
maalumu hivyo tunapenda kuwahamasisha kadi zetu za Debit na Cretid
kwenye tukio hili," alisema.
Kwa
upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa
Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na
kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.
“Nimefuarahi
sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es
Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa
kutambua umuhimu wangu.”
Msanii
huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu
hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye
tukio hili.
Kwa
hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha
kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa
Jombo.