Omran Daqneesh ni mmoja wa watoto watano waliojeruhiwa vibaya katika
mashambulio yaliyofanywa na ndege jana nchini Syria ambapo picha
zinamwonyesha akiwa amejaa vumbi baada ya kutolewa katika kifusi
kilichosababishwa na shambulio hilo.
Mtoto
huyo ambaye anaonekana kutokuwa na fahamu na akiwa ametapakaa damu na
akiwa amepakiwa katika gari la wagonjwa, ni kielelezo cha ukatili
unaofanyika katika mji wa Aleppo nchini Syria katika vita vya ndani
vinavyoendelea.
Picha
za video zinamwonyesha akiwa amepata fahamu huku damu ikimtoka na
akijaribu kupangusha vumbi usoni. Hata hivyo, anaendelea kusubiri ili
kupata tiba kutoka kwa madaktari.

Taswira
hizo za mtoto Omran zimeenea kwa haraka baada ya kuwekwa katika
mitandao ya jamii jana, wakati ambapo juhudi za kidiplomasia zinafanywa
ili kusimamisha mapigano hayo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alionya kwamba mji wa Aleppo unakabiliwa
na janga la kibinadamu hivi karibuni, na alizitaka Russia na Marekani
kufikia makubaliano ya haraka ya kusimamisha mapigano katika mji huo na
sehemu nyingine nchini humo