Pichani juu majeruhi katika milipuko hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza.
Mabomu hayo yalikuwa yamefichwa na kulipuliwa kwa kutumia simu za mkononi.
Milipuko miwili ya kwanza ililipuliwa katika mtaa wa kitalii wa Hua Hin usiku wa kuamkia leo na kuua mtu mmoja.
Milipuko mingine imetokea leo asubuhi katika mji ulio karibu na Bangkok huku milipuko mingine miwili ikilipuliwa katika kisiwa cha Phuket, ambapo ni maarufu kwa kuwa na watalii kutoka nje ya nchi.