Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena
baada ya Mahakama ya Rufaa kufuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia
mbali hoja za kupinga matokeo hayo, ambazo ziliwasilishwa na wafuasi
wanne wa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Steven Wasira (CCM).
Jaji Mohamed Gwae wa Mahakama Kuu,
alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukubali pingamizi la Lissu kuwa
wafuasi hao hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.
Wakazi hao wa Bunda wanadai kuwa
uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na kugubikwa na vitendo vya
rushwa, mgombea wanayemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo na
pia kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura.
Jana, Lissu, ambaye ni Mwanasheria
Mkuu wa Chadema na wakili wa kujitegemea, alitoa majibu ya utetezi mbele
ya Jaji Lameck Mlacha kuanzia saa 4.10 asubuhi na kukamilisha saa 6.02
mchana wakati shauri hilo lilipoahirishwa kwa muda hadi saa 8:00 mchana
kutoa fursa kwa mawakili wa upande wa wadai, Constantine Mutalemwa
kujibu.
Lissu alidai kuwa waleta maombi
wameshindwa kutoa hoja mahususi kuonyesha ukiukwaji wa sheria, kanuni na
taratibu za uchaguzi wanazodai ulikuwepo katika mchakato wa Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Wakili Lissu pia alidai kuwa
walalamikaji ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na
Ascetic Malegele, pia wameshindwa kuonyesha madhara waliyopata kama
wapigakura kuishawishi mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi
Bulaya dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe.
“Waleta maombi wanadai uchaguzi
haukuwa huru na haki, idadi ya wapigakura kutofautiana kwa kila kituo na
uwepo wa vitendo vya rushwa, lakini hawabainishi wazi nani mhusika wa
mambo wanayoyalalamikia na madhara waliyopata kwa nafasi yao ya
wapigakura,” alisema wakili Lissu.
Alisema vitendo vya rushwa katika
uchaguzi ni kosa kubwa linaloweza kusababisha kubatilishwa kwa matokeo
ya uchaguzi mzima, lakini walalamikaji wana wajibu wa kumtaja mhusika wa
vitendo hivyo ili kuipa mahakama fursa ya kutafsiri vyema sheria na
kutoa haki.
“Lakini madai ya juujuu tena ya
jumla kuwa aliyetoa rushwa ni wakala wa mteja wangu, hayakubaliki mbele
ya macho ya sheria kwa sababu mtu huyo hajulikani na jukumu la
kuthibitisha madai ni la mleta maombi na uthibitisho huo haumo kwenye
hati yao ya maombi,” alidai Lissu.
Aliomba maombi hayo yafutwe kwa hoja
kwamba wadai hawajataja vifungu vinavyoipa mahakama haki na mamlaka ya
kuyasikiliza na kuyaamua