Akizungumza na waandishi wa habari
jana Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa JWTZ Kanali Ngemela Lubinga
aliwatoa hofu wananchi kuwa wasitishike pindi watakapoona wanajeshi
katika maeneo ya karibu na makazi yao.
“Kesho (leo) tuaanza kufanya usafi
kuanzia maeneo ya Kawe hadi karibu na kambi ya Lugalo, na kwamba niwatoe
hofu wananchi pindi watakapoona wanajeshi wengi mitaani kwa kuwa hatuna
nia mbaya hivyo wasitufikilie vibaya,” alisema.
Alisema jeshi hilo litafanya usafi
pamoja na upandaji miti katika baadhi ya maeneo nchini hadi siku ya
kilele cha maadhimisho hayo. Pia wanajeshi watajitolea damu salama
katika hospitali za kambi za jeshi.
“Siku kuu ya majeshi itaadhimishwa
pamoja na wanajeshi kujitolea damu kwenye vituo maalumu vya kutolea damu
salama mikoani, katika hospitali zetu za kanda,” alisema na kuongeza.
“Sanjari na utoaji damu, madaktari
wetu JWTZ watatoa huduma za tiba bure kama upimaji wa virusi vya Ukimwi,
kisukari, na upimaji wa shinikizo la damu. “
“Kama ilivyo mila na desturi ya
majeshi kufanya usafi na utunzaji wa mazingira, kuelekea siku ya
maadhimisho tutafanya usafi na kupanda miti maeneo ya jirani na kambi na
kwenye taasisi za kiraia kadri mahusiano yatakavyofanyika na taasisi
hizo, ” alisema.
Pia alisema siku hiyo ya maadhimisho
itaadhimishwa kwa kuienzi michezo na kudumisha urafiki baina ya JWTZ,
wananchi, na Taasisi na kwamba mashindano mbalimbali yatafanyika.
Tarehe hiyo hiyo ya Septemba 1 , Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimetengaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima ili
kulaani kile wanachokiita udikteta unaofanywa na serikali ya awamu ya
tano.
Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.
Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.