Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi.

Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikagua ujenzi wa matundu ya choo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya
maendeleo katika kijiji cha Utaho A ambapo inajengwa shule mpya ili
kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo
pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari
kwao.
Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambacho kina jumla ya matundu 12.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani Mbeya