Wanafunzi wakiangalia vyoo wanavyovitumia
Wanafunzi wa Shule ya msingi Maendeleo
Manispaa ya Mtwara Mikindani wanalazimika kukosa sehemu ya vipindi vya
masomo darasanai kutokana na kupanga foleni kusubiri zamu ya kwenda
kujisaidia chooni.
Kwa upande wa walimu wa shule zote mbili, wamesema changamoto ya miundombinu ni kubwa katika shule hizo huku na wao ambao idadi yao jumla ni Zaidi ya 40 wakitumia matundu mawili ya choo cha shule moja, na kuiomba serikali na wadau wengine kuona umuhimu wa kutatua changamoto hizo.
Naibu Meya wa manispaa hiyo, Erick Mkapa ambaye ni diwani wa kata ya Rahaleo, amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa anafanya juhudi za kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha wanatatua tatizo hilo.