Patric Ole Sosopi (kushoto mwenye gwanda).
Dar es Salaam,
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana wa Chadema Taifa(BAVICHA), Patric Ole Sosopi leo amehojiwa Kituo
Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu
inayotishia uvunjifu wa amani.
Sosopi alifika kituoni hapo saa 4.10
asubuhi huku ameambatana na wakili wake Frederick Kikwelo huku
wakisindikizwa na wafuasi watano wa chama hicho.
Akizungumzia suala hilo baada ya kutoka
polisi mwanasheria wake alisema mwenyemkiti huyo alihojiwa kwa nusu saa
na alipewa dhamana na jeshi la polisi huku wakiendelea na upelelezi
wao ambapo ukikamilika watakabidhi kwa mwendesha mashtaka kwa ajili ya
kupitia ushahidi.
Sosopi alisema baada ya kuhojiwa
alielezwa na jeshi la polisi kuwa arudi Julai 18 mwaka huu lakini
hawajampa sababu ya msingi ya kurudi siku hiyo.
“Polisi hawajanipa sababu ya msingi ya kurudi Julai 18 mwaka huu,”alisema Sosopi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu alichohojiwa Sosopi, alisema
hana taarifa hizo hivyo atafuatiulia
chanzo: BOFYA HAPA