Riyama Ally
NA IMELDA MTEMA
DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu
anayekuja kwa kasi Bongo, Mwanaheri Ahmed hivi karibuni alikumbwa na
dhahama alipokatiza Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar baada ya
kuchaniwa dera lake kisa kufananishwa na muigizaji mwenzake, Riyama
Ally.
Mwanaheri Ahmed
Akizungumza na Amani Mwanaheri alisema
kuwa, amekuwa akikutana na sintofahamu kubwa njiani baada ya watu wengi
kumfananisha na Riyama hata kabla ya yeye kuingia kwenye uigizaji wa
filamu.
“Aisee hivi majuzi watu walichana mkono wangu wa dera wakiwa wananivuta na kuniita Riyama huko
Kariakoo na hata siyo hivyo tu hata
kabla sijaingia kwenye tasnia ya filamu wengi wananifananisha naye,”
alisema Mwanaheri anayebamba na filamu yake ya Mwanaheri