Waziri
wa habari utamaduni sanaa na michezo, Nape Nnauye amefanya ziara maeneo
ya Kariakoo kukagua na kukamata wanaotengeneza ‘kudurufu’ na kusambaza
‘kuuza’ CD ambazo hazina stika kutoka TRA na wala hazikupitishwa na bodi
ya filamu kusambazwa kwa wananchi.
Waziri
Nape baada ya kukagua maduka hayo amesema kuanzia sasa mtu yoyote
atakayenunua CD lazima aulize kama ina stika ya TRA kama haina asichukue
na endapo atachukua wote watakua na makosa ya kuhujumu uchumi na
watafikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi, katika zoezi
hilo Maduka zaidi ya 40 yamefungwa na bidhaa hizo zimechukuliwa
>>>’Kila
anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi
kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa
kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi
mwingine tutashyghulika na wewe‘ -Waziri Nape
