WATU sita kati ya 100
wanaoaminika kuwa ni memba wa kundi la kigaidi la Boko Haram waliokuwa
wakitafutwa na Jeshi la Ulinzi la Nigeria wamekamatwa wakiwa wamejificha
kanisanihuko Festac Jijini Lagos.
Zoezi hilo lilifanikiwa jana kutokana na
ushirikiano wa raia wema wa maeneo ya karibu kutoa taarifa kwa jeshi
hilo kuhusu kuwepo kwa watu waliyowatilia shaka wakiingia kwenye kanisa
hilo lililopo mjini Festac kwa lengo la kujificha ilihali muonekanao wao
sio wa kusali.
Washukiwa hao waliripotiwa kutafutwa na
jeshi hilo tangu wiki iliyopita baada ya kufanya shambulizi na kutokomea
huko mjini Maiduguri Borno.
Watuhumiwa waliokamatwa jana
wametamnbulika kwa majina ya Ali Ibrahim, Ahmed Abubakar, Kamsalem
Goigoi, Adams Ibrahim, Mohammed Ibrahim na Ali Blam Babagana waliokuwa
wakitoroka kutoka Borno walikotekeleza shambulio