Uzibuaji
wa Mitaro ukiendelea katika Mitaa mbalimbali ya Katikati ya Jiji la
Mwanza. BMG inatoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa halmashauri ya Jiji
la Mwanza kwa zoezi hili maana lisipofanyika kwa muda mrefu, mitaro hii
huziba, mvua inaponyesha huwa Mitaa ya Jiji haitamaniki tena na
inapoteza hadhi ya Jiji la Mwanza.