Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa
Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa
asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua
rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa
mauziano wa hisa hizo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya
mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za
kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), ambapo sasa inakuwa ikiimiliki TTCL kwa asilimia 100. Kulia
ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De
Faria (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye hafla ya kusaini mkataba wa
mauziano hayo. Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali wa TTCL
na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano walioshuhudia tukio hilo.
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akibadilisha hati ya mkataba wa
mauziano ya hisa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel
Afrika, Christian De Faria. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali
walioshuhudia tukio hilo.
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya
mauziano ya hisa. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti
Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu). Kulia ni Ofisa
Mkuu Mdhibiti wa Kampuni ya Bhart Airtel Afrika, Daddy Mukadi akiwa
kwenye hafla hiyo.
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (katikati) akizungumza katika hafla ya
kutiliana saini ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa
za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Maria Sasabo akiwa katika hafla
hiyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza
kulia).
Msajili
wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akijadiliana jambo na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De
Faria kwenye hafla ya kutiliana saini ya mauzo ya hisa asilimia 35
za kampuni ya Bharti Airtel leo Dar es Salaam.
Serikali kufanya marekebisho
ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki ili kuwezesha
watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za Mawasiliano kupitia
soko la hisa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni
Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
(Pichani)alipokuwa akiwasilisha Bungeni muswada wa Sheria ya Fedha ya
mwaka 2016.
“Mhe. Naibu Spika, sehemu ya nne
inapendekeza marekebisho katika sheria ya Posta na Mawasiliano ya
Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta kifungu cha 6(2d) na
kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za mawasiliano kuwasilisha
Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa umiliki wa hisa kama
mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha Mhe. Mpango aliendelea kwa
kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki watawekewa
sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na kusajili hisa zao katika soko la
hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa kwa watanzaniai kununua hisa na
kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana na marekebisho ya sheria
hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya kielektroniki ambazo tayari
zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika kujioredhesha katika soko la hisa
na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 01,
2016.
Vile vile kampuni ambazo zitasajiliwa
baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika kuuza hisa zao na kujioredheshsha
katika soko la hisa ndani ya kipindi cha Miaka miwili kuanzia Julai 01,
2016.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia amesema kwamba kamati
imekubaliana na marekebisho hayo aidha kamati inaishauri Serikali
kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha hisa hizo kuuzwa kwa
watanzania pekee na pia kuangalia suala la miezi sita kwa makampuni
yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji wake.