Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, John Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha
Muhas pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa
kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam mwishoni 
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, John Michael akizungumza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa nne wa
mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa ufungwaji wa Mkutano Mkuu wa nne
wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam .
Baadhi ya washiriki wa wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI
imesisitiza utafiti wa kisayansi kwa maendeleo ya taifa na kuhamasisha
ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi katika eneo hilo , ili kujenga
taifa lenye vijana watafiti na wataalam wa kutosha.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia hotuba yake
iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo John Michael
aliemuwakilisha kwenye ufungaji wa Mkutano wa nne wa mwaka wa utafiti
wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema
utafiti wa kisayansi ni muhimu kwa nchi yeyote ikiwemo Tanzania katika
kuhakikisha inafikia malengo yake ya maendeleo ya utekelezaji wa wa
malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGS).
Aliongeza
kuwa utafiti wa kisayansi ni kiungo muhimu katika kuweza kufikia
malengo ya SDGS kwa kuwa ndio unatoa muongozo wa kisayansi na mipango
ya namna ya kuyafikia malengo hayo.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Ephata Kaaya alisema ni
muhimu taifa kuanza kuchukua hatua sasa na kuhakikisha mfumo wa kitaifa
wa huduma za afya na uchumi kwa ujumla unaweza kukabiliana na mizigo
wa magonjwa , kwa njia ya utafiti.
Aidha
Prof Kaaya aliwapongeza wanafunzi wa shahada ya uzamili na wahitimu wa
MUHAS waliowasilisha mada takribani ya 70 kati ya 170 katika mkutano
huo na tofauti na mwaka uliopita ambapo asilimia 30 ya mada
ziliwasilishwa na wanafunzi.